Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limetangaza kuwa liko tayari kutoa jibu kali na la majuto kwa uchokozi au vitisho vyovyote kutoka kwa Marekani, Israel, au washirika wao. Taarifa hiyo imetolewa kwa mnasaba wa kumbukumbu ya siku 40 tangu kuuawa kwa makamanda wa IRGC katika uvamizi wa siku 12 wa Marekani na Israel.
IRGC imesisitiza kuwa operesheni ijayo dhidi ya adui itakuwa kali kuliko ilivyotarajiwa na yenye athari kubwa zaidi. Pia, imetaja kuwa Iran imepata uungwaji mkono wa kimataifa katika kulaani hujuma hizo za kinyama, na kwamba taifa la Iran halitasalimu amri kwa mashinikizo yoyote ya maadui.
Taarifa hiyo imehitimisha kwa kusisitiza kuwa ushindi wa Iran katika vita vya siku 12 umeimarisha heshima ya taifa na kufungua njia mpya ya kukabiliana na vitisho vya siku zijazo.
Iran iko tayari kwa Operesheni Kubwa Dhidi ya Wachokozi kwa muda wowote ule.
Your Comment